1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Real Madrid yasherehekea ubingwa wa Ulaya

Sekione Kitojo
5 Juni 2017

Maelfu ya mashabiki wa mabingwa wa kombe la Champions League Real Madrid waishangiria timu yao kwa kupata ushindi wa taji hilo kwa mara ya 12,wakiimba Cristian Ronald kutuzwa tuzo ya Ballon d'Or kwa mara ya tano.

https://p.dw.com/p/2e9FM
Juventus vs. Real Madrid - UEFA Champions League Final Pokal
Picha: Reuters/C. Recine Livepic

 

Ni shamra shamra zilizofana sana  jana  katika  uwanja  wa  Santiago Bernabeu  ambapo  maelfu  ya mashabiki walikusanyika  jana Jumapili kusherehekea  pamoja  na wachezaji  wao  taji  la  12 ambalo limekuja  baada  ya  kuishinda  Juventus Turin  siku  ya Jumamosi  mjini  Cardiff , Wales  kwa  mabao 4-1 na  kuwa  timu  ya kwanza  katika  bara  la  Ulaya  kuweza  kutetea  taji  hilo na kulinyakua  kwa  mara  ya  pili  mfululizo.

Wales Zinedine Zidane Championsleague-Trophäe
Kocha wa Real Madrid Zinedine ZidanePicha: Reuters/E. Keogh

Real madrid  imekuwa  timu  ya  kwanza  kulibakisha  kombe  hilo katika  kabati  lao  la  mataji  katika  mfumo uliopanuliwa  wa mashindano  hayo , na  kuonesha  uwezo  wake  na  nguvu  zao dhidi  ya  timu  nyingine  zote  barani  Ulaya.

Kocha  mkuu  wa  Real Madrid  Zinedine Zidane  ameweka  rekodi ya  kuwa  kocha  wa  kwanza   wa  klabu  hiyo kuweza  kunyakua mataji  mawili La Liga  na  Champions League katika  msimu  mmoja tangu  mwaka  1958 baada  ya  kuzima kitisho  cha  Barcelona kuweza  kunyakua   taji  la  ligi  ya  Uhispania. Mshambuliaji mahiri wa  timu  hiyo Cristiano Ronaldo  aliyefunga  mabao  mawili  katika mchezo  huo  wa  fainali alisema ulikuwa  msimu wa  kufurahisha sana.

"Moja, Mbili , Tatu ,(.....akishangiria....)  shukrani  nyingi  kwa kuwapo  hapa. Ukweli ni  kwamba  ulikuwa  msimu mzuri sana. Ningependa  kuwashukuru  wachezaji  wenzangu  wooote, makocha wetu . Tuko hapa  kusherehekea. Na shukrani  kwenu  nyie  kwa kuendelea  kutuunga  mkono. Asanteni  sana".

Wales Toni Kroos nach dem Championsleague-Finale
Mchezaji wa kati wa Real Madrid Mjerumani Toni KroosPicha: picture alliance/GES/M. Ibo Güngör

"Wachezaji  wameingia  katika  kundi la  wachezaji maarufu wa  Real Madrid  na  soka, kama  ilivyo  kwa  kocha  wetu," amesema  rais wa  klabu  hiyo Florentino Perez, wakati  akitoa  sifa maalum  kwa Zinedine  Zidane.

Zidane , ambaye  ni  Mfaransa , ambae  binafsi  alishinda  taji  hilo la  Champions League  akiwa  mchezaji  lejendari  kwa  Real  kati  ya mwaka  2001 na  2006, amepata  mafanikio  makubwa  tangu kuingia  katika  jukumu  lake  hilo  la  juu kuiongoza  timu  hiyo miezi 18  iliyopita.  Nae  alisema.

"Tumekuwa  na  mwaka  mzuri  sana na  nawashukuru  nyie  wote mashabiki kwasababu  mlituamini tangu  mwanzo  na tumeweza kushinda  mataji mawili."

Atmo: We are the  champions.......

 

Mwandishi: Sekione  Kitojo / dpae / afpe / ape / rtre

Mhariri: Iddi Ssessanga