1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Riadh. Watuhumiwa kadha wakamatwa kabla ya kufanya shambulio.

3 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCnE

Maafisa nchini saudi Arabia wamesema kuwa wamezuwia shambulio, baada ya kuwakamata zaidi ya watuhumiwa 130 katika muda wa miezi mitatu iliyopita.

Wizara ya mambo ya ndani imesema kuwa watuhumiwa, wengi wao wakiwa ni raia wa Saudia , wanahusiana na vikundi ambavyo vina maingiliano na mtandao wa kigaidi wa Al Qaeda. Wameongeza kuwa kikundi kimoja kilikuwa kinapanga shambulizi hivi karibuni.