1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RICHMOND : Mahkama yaamuru kuachiliwa mpiganaji adui

12 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBsZ

Mahkama nchini Marekani imesema Rais George W. Bush hawezi kuliamuru jeshi kuendelea kumshikilia kwa muda usiojulikana anaetuhumiwa kuwa mwanachama wa kundi la Al Qaeda.

Mahkama ya Rufaa huko Richmond katika jimbo la Virginia imeamuru kwamba raia wa Qatar Ali Saleh al- Marri aachiliwe huru kutoka mahabusu ya kijeshi.Mahakimu wametowa hukumu kwamba al-Marri anaweza kushtakiwa kwa madai ya uhalifu katika mahkama ya kiraia au arudishwe kwao.

Marri amekuwa katika mahabusu kama mpiganaji adui katika kambi ya wanamaji huko Charleston jimbo la Carolina ya Kusini tokea mwaka 2003.

Uamuzi huo ni pigo jengine kwa vita vya ugaidi vya utawala wa Bush.

Wiki iliopita madai dhidi ya watuhumiwa wawili wa ugaidi wanaoshikiliwa katika gereza la Marekani huko Guantanamo nchini Cuba yalitupiliwa mbali.