1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RIGA :Serikali itabakia madarakani kwa awamu ya pili

8 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD4p

Serikali ya muungano nchini Latvia,imeshinda chupu chupu uchaguzi wa bunge uliofanywa siku ya Jumamosi.Muungano wa vyama vya sera za kati na kulia chini ya uongozi wa waziri mkuu Aigars Kalvitis umepata kama asilimia 45 ya kura na jumla ya viti 51.Hii ni mara ya kwanza kwa serikali iliyo madarakani nchini Latvia, kuchaguliwa kwa awamu ya pili kwa mfululizo tangu nchi hiyo kupata uhuru wake mwaka 1991.Kalvitis alitoa ahadi kwa raia wake,kuwa atafanya matayarisho ya kuanza kutumia sarafu ya Euro.