1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RIO DE JANEIRO: Majeshi yaagizwa kukabiliana na ghasia za magenge mjini humo.

5 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCd8

Rais Luiz Inacio Lula da Silva ameyaagiza majeshi ya nchi hiyo kuingilia kati mjini Rio de Janeiro kukabiliana na ghasia za magenge ambazo zimesababisha vifo vya watu takriban ishirini.

Rais huyo amezitaja ghasia hizo kuwa vitendo vya kigaidi.

Amani imerejea mjini humo lakini ghasia za hapa na pale zimearifiwa kutokea.

Mji wa Rio de Janeiro unatarajiwa mwezi huu kuandaa mkutano wa wa marais wa mataifa ya Amerika kusini yanayoshirikiana kibiashara.

Mnamo mwaka elfu mbili na tatu, askari jeshi elfu tatu walipelekwa mjini Rio de Janeiro wakati wa karnivali baada ya magenge ya watu kuteketeza mabasi na kuwaua askari polisi saba na kusababisha maduka kufungwa.