1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ripota wa Deutsche Welle afukuzwa Tchechenya

16 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCio

Moscow:

Maafisa wa Urusi wamemfukuza ripota wa Deutsche Welle toka Tchechnya.Mwandishi habari huyo alitaka kuripoti juu ya shughuli za shirika linalowahudumia wakimbizi katika mji mkuu wa Tchechnya-Grosny.Ripota huyo wa Deutsche Welle amepokonywa kitambulisho chake cha uandishi habari na simu yake ya mkono .Kwa mujibu wa ripota huyo ,idara ya upelelezi wa ndani ya Urusi haikupendezewa kumuona anafanya kazi yake bila ya kufuatana na maafisa wa serikali.