1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ripoti: Manchester United yamfuta Van Gaal

23 Mei 2016

Kocha wa Manchester United Louis Van Gaal amefutwa kazi. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari nchini Uingereza. Klabu hiyo haijatoa tangazo lolote kuhusiana na habari hizo.

https://p.dw.com/p/1It8n
Großbritannien Manchester United Trainer Louis Van Gaal
Picha: picture-alliance/dpa/N. Roddis

Rpoti zinasema kuwa Mholanzi huyo amepigwa kalamu na kuwa Jose Mourinho, kocha wa zamani wa Real Madrid na Chelsea anatarajiwa kuchukua nafasi yake.

Shirika la habari la BBC liliripoti kwa mara ya kwanza kuhusu habari hizo siku ya Jumamosi mara tu baada ya Manchester United kushinda Kombe la Shirikisho la Kandanda Uingereza , FA. United iliifunga Crystal Palace mabao mawili kwa moja katika fainali iliyochezwa uwanjani Wembley.

Ripoti za vyombo mbalimbali vya habari nchini Uingereza na Uhispania zinasema kuwa wakala wa Jose Mourinho, Jorge Mendes anatarajiwa kuwasili Uingereza wakati wowote ili kukamilisha mkataba huo kabla ya tangazo rasmi kutolewa baadaye wiki hii

Mwandishi: Bruce Amani/DPA/AFP
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman