1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ripoti ya OECD juu ya ufukara

22 Oktoba 2008

Hali ya elimu na kuzidi ufukara Ujerumani ni miongoni mwa mada zilizochambuliwa:

https://p.dw.com/p/Feiw

Safu za wahariri wa magazeti ya Ujerumani, leo zimechambua mada mbali mbali-kuanzia ripoti iliotoka jana ya shirika la OECD juu ya kuongezeka mwanya kati ya matajiri na masikini nchini Ujerumani;mkutano wa kilele juu ya hali ya elimu nchini,msukosuko wa fedha hadi hotuba ya jana ya rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy,katika Bunge la ulaya huko Strassbourg juu ya msukosuko huo na jinsi ya kupata dawa ya kuutibu.

Gazeti la Landeszeitung kutoka Luneburg likiichambua ripoti ya shirika la OECD laandika:

"Shirika la OECD kwa mara nyengine tena limetoa ripoti mbaya kwa Ujerumani.Kwani, limesema hakuna nchi nyengine ilioendelea kiviwanda ambako kiwango cha umasikini kinaongezeka zaidi kama nchini Ujerumani.Na hasa wananchi wanaoishi pekee yao na watoto ndio walioathirika mno na ufukara huo wa kuaibisha.Tofauti na ripoti ya hali ya elimu nchini PISA,hakuna kisingizio kuwa tarakimu zilizotolewa jana ni za kale na kuwa eti hali imetengenea,la hasha."

LANDESZEITUNG linaongeza kuandika kuwa, tangu 2005 ingawa ukosefu wa kazi ulipungua.....ukweli tarakimu zaonesha maalfu waliojipatia kazi hizo ni za muda tu na za malipo ya chini.Kupanda kwa bei za vitu kumemeza hata mapato yao na kuwaweka katika hali za kufadhahika kimaisha.Wengi wao,laandika gazeti-wanakabiliwa na msiba wa ufukara.

Likiendeleza mada hii, gazeti la Neuste Nachrichten kutoka Dresden laandika:

"Taarifa za kustusha hazimaliziki.Haukupita muda tangu serikali ya Ujerumani kupitisha mpango wake wa kiinua-mgongo kwa mabenki ya ujerumani ba kuyaokoa kufilisika ili pia kurejesha imani ya wananchi ,taarifa ya shirika la OECD imetoka ikibainisha mwanya unaozidi kukua kati ya ukosefu wa usawa baina ya mapato ya wachache na wengi.Wataalamu wa sayansi ya jamii wa shirika hilo wanailaumu serikali kushindwa kuwa na sera bora tangu za soko la kazi hata sekta ya elimu.

Badala ya kuchunguza barabara ripoti hiyo na kuzingatia nini la kufanya kurekebisha hali ya mambo na kutafuta chanzo kilichopelekea hali hii,wanasiasa wanarejea desturi yao ile ile ya kutlaumiana na kutupiana jukumu."

Likizungumzia mkutano wa kilele ulioitishwa leo juu ya hali ya elimu nchini tena katika kipindi hiki cha msukosuko wa fedha, gazeti la BILD linalochapishwa Berlin lauliza:

"Je, kuitisha mkutano huo katika kipindi hiki cha msukosuko wa fedha na mifuko mitupu kunastahiki ?" jibu lasema gazeti ni ndio.Kwani,laongeza, Ujerumani bila elimu bora na ya hali ya juu ni sawa na Saudi Arabia bila ya mafuta ya petroli.Itageuka masikini kabisa.

Elimu yapasa kuwa jukumu la usoni kabisa kwa taifa.Ikiwsa serikali za mikoa ya ujerumani zimejifunza darasa lao kutoka ripoti ya (PISA) basi ni uzuri.Lakini, haitoshi tu kujifunza ikiwa Ujerumani iwe mionongoni mwa nchi zilizoendelea kabisa kielimu duniani.Wakati umewadia wa kupiga hatua ya pili......

Kusoma, husoma yule alietia nia ya kusoma na mwenye mtu wa kumpigia mfano ili awe kama yeye.Hii ina maana: Serikali ya shirikisho,zile za mikoa na miji haziwezi kutimiza jukumu hilo pekee yao.Pia mchango wa baba,mama na ukoo unatakiwa.Kwani, haw andio wa kwanza wanaowaelimisha watoto wao.Elimu ina thamani zaidi ya fedha.

Likiturejesha katika msukosuko wa fedha ulioibuka karibuni,gazeti la MannheimerMorgen laandika:

"Ni sawa kwa serikali ya Ujerumani kudai kuwa na ushawishi wake katika shughuli za mabaenki endapo banki hizo zinahitaji fedha za kutiwa jeki na serikali.Swali lakini, ni je, hali itakuwa bora pale wamangimeza wakigeuka wanabanki ?

........................yabainika kana kwamba uchumiwa soko huru unaowahurumia pia wanyonge unapaswa kulindwa usimezwe na mapapa wakubwa wa ubepari lakini wakati huo huo pia na mkono mwingi wa umangimeza wa dola."