1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RIYADH:Kansela Merkel aendelea na ziara ya mashariki ya kati nchini Saudi Arabia

5 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCUs

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani yupo nchini Saudi Arabia kuendelea na ziara ya siku nne katika mashariki ya kati.Kansela Merkel anafanya ziara hiyo kwa lengo kuzitia msukumo mpya juhudi za kuanzisha tena mazungumzo ya kuleta amani baina ya wapalestina na waisraeli.

Bibi Merkel amewasili Saudi Arabia kutokea Misri ambapo alifanya mazungumzo na katibu Mkuu wa Umoja wa nchi za Kiarabu bwana AMR MOUSSA na rais Hosni Mubarak.

Kiongozi huyo wa Ujerumani pia atazitembelea Umoja wa Falme za Kiarabu na Kuwait.