1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RIYADH:Khatoum yaendelea kukataa kupelekwa jejshi la UN huko Darfur

29 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCEg

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon hapo jana amefanya mazungumzo na Rais Omar Al Bashir wa Sudan kujaribu kumshawishi kiongozi huyo kukubali kupelekwa kwa jeshi la umoja huo la kulinda amani huko Darfur.

Mazungumzo hayo yalifanyika pembezoni mwa mkutano wa wakuu wa nchi za kiarabu, saa chache baada ya Rais Bashir kukataa katakata kupelekwa kwa kikosi hicho cha Umoja wa Mataifa.

Ban Ki-Moon anajaribu kupata msaada wa wakuu wa nchi za kiarabu katika kuushawishi utawala wa Khatoum kuruhusu kupelekwa kwa kikosi hicho kuungana na kile cha Umoja wa Afrika katika eneo lenye mzozo la Darfur.

Katika hotuba yake kwenye mkutano huo, Rais Omar Al Bashir alikataa kupelekwa kwa kikosi cha askari elfu 20 wa Umoja wa Mataifa, akisema kinachotakiwa kufanywa na Umoja huo ni kutoa msaada wa fedha na vifaa kwa jeshi la Umoja wa Afrika ambalo liko huko Darfur.