1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Robert Zoellick ni Rais mpya wa Benki ya Dunia

27 Juni 2007

Robert Zoellick sasa ndiye rais mpya wa benki ya dunia baada ya kuidhinishwa hapo jana na bodi ya magavana ya benki hiyo.

https://p.dw.com/p/CHC8
Bw.Robert Zoellick na Bibi Heidemarie Wieczorek-Zeul,waziri wa misaada na maendeleo wa Ujerumani, walipokutana mjini Berlin.
Bw.Robert Zoellick na Bibi Heidemarie Wieczorek-Zeul,waziri wa misaada na maendeleo wa Ujerumani, walipokutana mjini Berlin.Picha: AP

Zoellick alikuwa mwanadiplomasia wa Marekani na vile vile mjumbe katika masuala ya biashara. Raisi huyo mpya wa Benki ya Dunia anachukuwa mahala pa Bwana Paul Wolfowitz aliyekubali kung'atuka kwenye wadhifa huo baada ya kukabiliwa na kashfa ya kumpendelea mpenzi wake wa kike.

Je kuchaguliwa kwa Robert Zoellick kuongoza taasisi hiyo muhimu duniani kunaangaliwa vipi na wanauchumi barani Afrika. Saumu Mwasimba alimuuliza Balozi Ami Mpungwe, kaimu mwenyekiti wa benki ya taifa ya biashara Tanzania ya NBC.