1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROMA:Mshauri mkuu mpya wa Iran katika suala la Nuklia akutana na Solana

23 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7DM

Mkuu wa sera za nje katika Umoja wa Ulaya Javier Solana anakutana leo hii na mjumbe mpya wa Iran katika mazungumzo ya Nuklia bwana Saeed Jalili aliyeteuliwa wiki iliyopita baada ya kujiuzulu kwa Ali Larijani.

Jalili ni mshirika wa karibu war ais wa Iran Mahmoud Ahmedinejda na kwahivyo wanadiplomasia wa Ulaya watajaribu kuangalia iwapo kuna mabadiliko yoyote ya sera za Iran kuelekea suala la Kinuklia.

Mjumbe wa zamani wa Iran katika mazungumzo hayo Ali Larijani pia anatarajiwa kuwa mjini Roma kwa mazungumzo hayo.

Larijani alijiuzulu mwishoni mwa wiki kufuatia hali ya kutoelewana baina yake na rais Ahmadinejad kuhusiana na mazungumzo.