1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Romano Prodi aondoka Afghanistan

23 Desemba 2007

---

https://p.dw.com/p/CfVw

KABUL:

Waziri mkuu Romano prodi wa Itali, ameondoka Afghanistan leo baada ya ziara yake fupi iliojumuisha mazungumzo na rais Hamid Karzai wa Afghanistan pamoja na mkutano na wanajeshi wa Itali. Prodi alisherehekea misa ya X-masi na wanajeshi 1000 wa kitaliana mjini Kabul.

Ziara ya Bw.Prodi ilitanguliwa na ile ya rais Sarkozy wa Ufaransa na ya waziri mkuu mpya wa Australia.

Waziri mkuu wa Australia Kevin Ruud kabla kuondoka aliihakikisha Afhanistan kuwa vikosi vya Australia huko vitatimiza jukumu lake.Alisema


„Tumebeba jukumu hapa la wanajeshi wetu na tunataka kutumia fursa hii bila kuchelewa kuwatembelea kuihakikishia serikali ya Afghanistan kuwa jukumu letu linasalia pale pale.“

Alisema waziri mkuu wa Australia.