1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROME: Rais wa Afghanistan ziarani nchini Italia

16 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCRd

Rais Hamid Karzai wa Afghanistan akiwa ziarani nchini Italia,hii leo anakutana na waziri mkuu Romano Prodi na Rais Giorgio Napolitano mjini Rome.Prodi anaeongoza serikali ya mseto ya Italia,ameamua kuwabakisha wanajeshi wa Kitaliana wapatao kama 1,800 nchini Afghanistan,licha ya upinzani wa chama cha kikomunisti ambacho ni sehemu ya serikali hiyo ya mseto.Lakini,Prodi amekataa ombi la NATO la kuongeza idadi ya wanajeshi wake nchini Afghanistan.Hata rais George W.Bush siku ya Alkhamisi alitoa wito kwa washirika wa NATO kutoa mchango zaidi wa kijeshi nchini Afghanistan.