1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Cristiano Ronaldo alia viwanja kuendelea kuwa vitupu

Deo Kaji Makomba
9 Septemba 2020

Mchezaji nyota wa soka ulimwenguni Cristiano Ronaldo, amelilinganisha soka katika viwanja vitupu visivyokuwa na mashabiki kama kwenda kwenye sarakasi bila na kuwa na vazi rasmi la kuchekesha.

https://p.dw.com/p/3iEcq
Champions League - Juventus v Olympique Lyonnais | Cristiano Ronaldo
Picha: Imago Images/Gribaudi/ImagePhoto

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ureno, alifunga bao lake la 100 na 101 kwa nchi yake katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Sweden Jumanne (08.09.2020) katika ligi ya soka ya mataifa.

"Ni kama kwenda kwenye sarakasi bila mchekeshaji aliyevalia vazi la kuchekesha katika, kwenda kwenye bustani bila maua," alisema Ronaldo na kuongeza, "Hatupendi kama wachezaji, lakini tayari nimezoea. Ninatafakari kabla ya mechi tayari nikijua kuwa uwanja utakuwa mtupu."

Fußball Champions League I Juventus vs Olympique Lyonnais
Cristiano Ronaldo uwanjaniPicha: Reuters/M. Pinca


Ronaldo alisema kuwa amekosa hata mashabiki wapinzani. "Inasikitisha," alisema mshambuliaji huyo wa klabu ya Juventus ya Italia. "Ninapenda wakati ninapodhihakiwa katika mechi za ugenini, inanipa motisha. Lakini suala la afya linatakiwa kupewa kipaumbele na tunahitaji kuheshimu hilo. Lakini inasikitisha."

Aidha Ronaldo alisema ana matumaini kuwa "ndani ya miezi michache”mashabiki wanaweza kurudi viwanjani kwa sababu wao ndio "furaha” ya mchezo wa soka.

Kwa magoli yake dhidi ya Sweden, Ronaldo amekuwa mchezaji wa pili tu wa kiume kufikia magoli 100 katika mpira wa miguu wa kimataifa. Anamfuatia tu mshambuliaji wa zamani wa Iran, Ali Daei, ambaye aliifungia timu yake ya taifa mabao 109.

Chanzo: AP