1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rosberg ashinda mkondo wa Ujerumani

21 Julai 2014

Lewis Hamilton anaweza kuyarekebisha haraka makosa aliyofanya na kumruhusu mwenzake wa Mercedes, Nico Rosberg, kuchukua usukani katika mkondo wa wikendi ijayo wa Hungarian Grand Prix.

https://p.dw.com/p/1CgGh
Nico Rosberg Großer Preis von Deutschland 20.7.2014
Picha: picture-alliance/dpa

Madereva hawana muda wa kutosha kupumzika kutokana na kivumbi cha mashindano ya mkondo wa Ujerumani – German Grand Prix, ambapo pengo kati ya Rosberg na Hamilton ni pointi 14 katika orodha ya kinyang'anyiro cha ubingwa wa madereva.

Mjerumani Rosberg aliendesha gari lake bila kufanya makosa yoyote kutoka mwanzo hadi mwisho kwenye ardhi ya nyumbani mwishoni mwa wiki, huku naye Hamilton akianza katika nafasi ya 20 na kumaliza wa tatu nyuma ya dereva Valtteri Bottas wa timu ya Williams.

Rosberg anasema anasubiri kwa hamu mashindano ya Hungary huku akikipongeza kikosi chake cha Mercedes kwa kutengeneza gari linalompa uwezo wa kushinda kwa urahisi.

Mwandishi: Bruce Amani /DPA/AFP
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman