1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROSTOCK: Ahadi za kuongeza misaada Afrika zitekelezwe

8 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBtr

Watu 80,000 wamehudhuria tamasha la muziki lililofanywa Alkhamisi mchana mjini Rostock, kaskazini mwa Ujerumani.Lengo la tamasha hilo ni kuwakumbusha viongozi wa kundi la madola tajiri manane G-8 wanaokutana mji wa jirani wa Heiligendamm,watimize ahadi walizotoa mwaka 2005 kuwa misaada ya maendeleo barani Afrika, itaongezwa maradufu ifikapo mwaka 2010.Kama waimbaji na makundi 20 mbali mbali ya muziki yalishiriki katika tamasha hilo,ikiwa ni pamoja na mwanamuziki mashuhuri wa Kijerumani Herbert Grönemeyer,Bono wa kundi la U2 na Bob Geldof wa Uingereza alie maarufu kwa juhudi zake za kukusanya misaada ya kupiga vita njaa na umasikini barani Afrika.