1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROSTOCK : Maadamano ya ghasia dhidi ya kundi la G8

3 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBvN

Zaidi ya polisi 140 wamejeruhiwa katika mapambano ya matumizi ya nguvu na waandamanaji wa sera kali za mrengo wa shoto waliokuwa wakiwavurumishia mabomu ya petroli hapo jana kabla ya kufanyika kwa mkutano wa viongozi wa kundi la Mataifa Manane G8 wiki ijayo.

Ghasia hizo zimezuka wakati maelfu ya watu walipoandamana katika mji wa bandari wa kaskazini mashariki ya Ujerumani wa Rostock ulioko kama kilomita 25 kutoka mji wa kitalii wa Heilligendam ambapo wakuu wa mataifa hayo tajiri kabisa duniani wataanza mkutano wao wa siku tatu hapo Jumatano.

Polisi imesema waandamanaji 78 wametiwa mbaroni na polisi 146 wamejeruhiwa 25 kati yao ikiwa wamejeruhiwa vibaya sana. Polisi ilitumia maji kuwatawanya waandamanaji hao waliokuwa wameziba nyuso zao ambao walikuwa wakiwavurumishia polisi mabomu ya petroli na mawe.

Magari kadhaa yametiwa moto na mengine kupinduliwa juu chini.

Takriban wanaadamanaji 30,000 walianza maandamano hayo kwa amani kauli mbiu yao ikiwa inawezekana kuwa na dunia aina nyengine wakidai msaada kwa Afrika na kuchukuliwa kwa hatua dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa.

Kundi linalopinga utandawazi la Attac limejitenganisha na waandamanaji hao.