1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROSTOCK:Waandamanaji wapambana na polisi Rostock

4 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBuo

Waandamanaji wamepambana na polisi kabla ya mkutano wa kilele wa kundi la mataifa manane yaliyostawi kiviwanda G8 kufanyika wiki hii.Waandamanaji hao wanapinga hatua ya maafisa wa usalama wa Ujerumani ya kuzuia idadi ya watu kufika katika eneo la mkutano mjini Heiligendamm.

Takriban waandamanaji 800 walikusanyika nje ya afisi za uhamiaji katika eneo la Rostock wakidai uhuru wa kutembea bila vikwazo na haki sawa kwa wote wakiwemo wakimbizi na wanatafuta hifadhi.

Kwa mujibu wa mtandao wa Spiegel mpiga picha mmoja wa habari alijeruhiwa na watu wengine wane kuzuiliwa pale waandamanaji 400 walipopambana na polisi.Waandamanaji wengine alfu 20 wanatarajiwa kufanya maandamano mengine ya kupinga mkutano huo wa G8 mjini Rostock leo baadaye.

Wakati huohuo mahakama kuu hapa Ujerumani inatangaza hii leo kuwa kundi moja la wanaharakati linakata rufaa kuhusu uamuzi wa mahakama moja wa kupinga maandanamo nje ya mji wa Heiligendamm.Uamuzi huo badala yake uliatoa ilani ya kupiga marufuku watu kufika karibu na mkahawa kutakakofanyika mkutano huo na kuzungushia mji wa Heiligendamm uzio wa kilimita 11.