1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ruanda: Wafungwa wagoma kutokana na huduma mbaya ya Chakula

28 Septemba 2009

<p>Maelfu ya wafungwa katika magereza mawili makubwa nchini Rwanda walifanya mgomo na vurugu mwishoni mwa juma, wakilalamikia huduma mbaya ya chakula.

https://p.dw.com/p/JsTw
Rwanda ambako wafungwa wagoma kwa ajili ya hali mbaya ya chakulaPicha: James Nzibavuga
Katika gereza la Rusizi kusini mwa nchi hiyo wafungwa walisema matatizo ya chakula yamekuwepo kwa muda wa mwezi mzima. Viongozi wa magereza nchini humo wamekiri kutokea matatizo ya chakula, lakini wakasisitiza kuwa machafuko yalichochewa na wafungwa wenye vurugu. Kwa sasa hali imetulia baada ya mazungumzo baina ya pande zinazohusika.

Mwandishi wetu kutoka Kigali, Rwanda, Daniel Gakuba ana maelezo zaidi:

Mwandishi: Daniel Gakuba

Mtayarishaji: Grace Patricia Kabogo

Mhariri: Thelma Mwadzaya