1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rwanda: Mkutano kuhusu Adhabu ya Kifo

24 Septemba 2009

Umoja wa Afrika -AU- umeanzisha mjadala kuhusu adhabu ya kifo, kwa lengo la kuzishawishi nchi wanachama wake kufuta adhabu hiyo, ambayo umoja huo unasema inakiuka haki ya binadamu kuwa na uhai.

https://p.dw.com/p/JoG6

Mojawapo ya mijadala hiyo umeanza mjini Kigali nchini Rwanda, ukiwahusisha wanaharakati wa haki za binadamu kutoka Afrika ya Mashariki, Kati na Kusini.

Kaimu kamishna wa Tume ya AU ya haki za binadamu, Bahami Tom Nyanduga ambaye anauongoza mjadala huo, amesema lengo la umoja wa Afrika ni kufikia itifaki itakayozilazimu nchi wanachama wote kuiondoa adhabu kwenye sheria zake siku za usoni.

Daniel Gakuba amehudhuria mkutano huo na kututumia taarifa ifuatayo.