1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SADC imesitisha mkutano wake kufuatia hofu ya Corona

Amina Mjahid
10 Machi 2020

Nchi wananchama wa Jumuia ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC, zimesitisha mkutano wa ana kwa ana wa Baraza la Mawazi wa Fedha na Mipango kutokana na hofu ya virusi vya Corona, mkutano huo utafanyika kwa mfumo wa video.

https://p.dw.com/p/3Z8BE
Tansania südafrikanische Präsident Cyril Ramaphosa (links) und der tansanische Präsident John Pombe Magufuli
Picha: DW/Eric Boniface

SADC imesitisha mkutano wake kufuatia hofu ya Corona

Hatua hiyo imefikiwa baada ya mawaziri wananoshughulikia sekta ya Afya katika jumuia hiyo kuketi kwa dharura hapo jana na kujadili hali halisi ya COVID-19 duniani na katika nchi wananchama na maandalizi ndani ya jumuia katika kukabiliana na virusi hivyo pamoja na hatua za kuchukuliwa kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo.

Virusi vya Corona tayari umekwisha shambulia takriban mataifa 101 ulimwenguni kati ya mataifa 194. 

Sehemu ya makubaliano ya mawaziri wa afya ni kuzuia mikutano ambayo inaweza kuzuilika hivyo kuafiki mkutano wa baraza la mawaziri wa fedha, mipango, viwanda, biashara na mambo ya nje kufanyika kwa njia ya video ambapo kila mshiriki atakuwa nchini mwake wakati mkutano ukiendelea.

SADC imesitisha mkutano wake kufuatia hofu ya Corona

Akitoa taarifa ya kubadilishwa kwa mfumo huo wa mkutano katibu mkuu wizara ya mambo ya nje nchini Tanzania balozi kanali Wilbert Ibughe amesema utaratibu huo wa kuendesha mkutano kwa njia ya video umeridhiwa na sekretarieti ya SADC pamoja na nchi mwenyekiti kwa kuwa unalenga kuondoa hatari ya kuenea kwa ugonjwa endapo mmoja kati ya washiriki atakuwa amepata maambukizi.

Tanzania President John Pombe Magufuli in Dar es Salaam
Picha: DW/S. Khamis

"Sasa kufuatia ushauri uliotolewa katika maazimio ya kikao cha mawaziri wa afya wa SADC jana, kikao cha baraza la mawaziri wa SADC  kilichokuwa kimepangwa kimefupishwa na sasa kitaafanyika kwa njia ya video tarehe 18," alisema balozi kanali Wilbert Ibughe.

Tanzania imezitaka serikali za SADC kuchukua hatua zinazopendekezwa na wataalamu wa afya ili kujikinga na Corona

Ikumbukwe kuwa utaratibu huu wa kufanya mkutano kwa njia ya video kwa jumuia hiyo utakuwa ni wa kwanza kufanyika ambapo Tanzania kama mwenyekiti imezitaka serikali za SADC kuchukua hatua stahiki zinazopendekezwa na wataalamu wa afya ili kujikinga na ugonjwa huo hatari ambao tayari nchi mwananchama wa SADC Afrika kusini imethibitisha kuwepo kwa wagonjwa takriban saba.

Logo von SADC

Naibu katibu mkuu mtendaji anaeshughulikia utengamano wa SADC dokta Tembikosi Mpongo amewaambia wanahabari kuwa kama jumuia inafanya kila linalowezekana kuhakikisha wanalinda afya za wakaazi ikiwemo kuepuka mikusanyiko inayohatarisha kuenea kwa ugonjwa huo.

"Kipaumbele cha kwanza cha serikali ni kuwakinga watu wake na hivyo tunafanya kwa kuzuia makutano ya aina kwa ana yasio ya lazima ambapo maambukizi yanaweza kutokea, hii si kwetu tu ni ulimwegu mzima umechukua hatua kama hii  ili inapotokea hatua za haraka zinachukuliwa kukabiliana lakini kwanza ni kudhibiti kadri inavyowezekana," alisema dokta Tembikosi Mpongo

Tangu kuzuka kwa Virusi vya COVID-19 ama Corona mwishoni mwa mwaka uliopita tayari vimeshaua zaidi ya 3,100 nchini china, 463 Italia na barani Afrika, Misri imeripoti kifo cha kwanza kutokana na ugonjwa huo na nchi kadhaa zimethibitisha kupatikana kwa wagonjwa walioambukizwa virusi hivyo ikiwemo Afrika kusini, Nigeria, Algeria pamoja na Senegal.

Chanzo: Hawa Bihoga DW Dar es salaam