1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merkel ahimiza mjadala wa kuheshimiana

Sekione Kitojo
31 Desemba 2017

Katika hotuba yake  ya  kuukaribisha  mwaka  mpya , kansela  Angela  Merkel ametoa  wito kwa  Wajerumani  kuonesha  mshikamano  na  kuheshimiana wakati  wakitofautiana katika majadiliano ya  kisiasa.

https://p.dw.com/p/2q9Zf
Deutschland | Neujahrsansprache BK Angela Merkel 2018
Picha: picture-alliance/dpa/H. Hanschke

Katika  hotuba  yake , ambayo itatangazwa  katika televisheni  ya  taifa leo Jumapili  jioni, merkel   hakutumia  maneno  mengi  kabla  ya  kuelezea wasi wasi  wake  juu  ya  umoja  katika  jamii  ya  Wajerumani.

"Hakujawahi  kuwa  na  tofauti  ya  mawazo  kama  hayo kwa  muda  mrefu." amesema. " Baadhi  hata wanafikia wanazungumzia kuhusu  kuvunjika  kwa mshikamano  wa  jamii  yetu."

Deutschland Angela Merkel macht Selfie auf Fest in Stralsund
Merkel anahimiza Wajerumani kuwa na Umoja zaidiPicha: Getty Images/S. Gallup

Lakini mafanikio na uaminifu  ni  sehemu ya uhalisia  wa  Ujerumani  kama hofu  na  wasi wasi, amesisitiza, na  kuongeza: "Kwangu mimi , mambo  yote hayo mawili  yananihusu."

Merkel  amesema  kwamba  Wajerumani  wanahitaji "kutambuana  zaidi, na nina maana kutambuana kweli - tusikilizane, tusikilize hasa, tuoneshe kuelewa."

Kiongozi  huyo  mwenye  umri  wa  miaka  63, ambaye  kwa sasa  anaongoza serikali  ya  mpito baada  ya  uchaguzi  wa  mwezi  Septemba kusababisha mkwamo  wa  kisiasa, pia  alitumia hotuba  hiyo  kama  fursa ya kuwahakikishia  Wajerumani kwamba  anataka  kuunda  serikali  imara haraka iwezekanavyo.

Deutschland Berlin - Angela Merkel und Martin Schulz
Merkel (Kushoto) na kiongozi wa chama cha SPD Martin SchulzPicha: Reuters/A. Schmidt

Serikali ya mseto

Vyama  viwili  vikubwa  nchini  Ujerumani , chama  cha  Christian Democratic Union CDU  na  kile  cha  Social Democratic SPD, vilipata  pigo kwa kupoteza kwa  kiasi  kikubwa  katika  uchaguzi  wa  Septemba  24. Chama cha  SPD awali  kilikataa  kushitiki  katika  serikali  mpya ya  muungano  mkuu na  wahafidhina  wakiongozwa  na  Merkel, lakini  hivi  sasa  kinatafakari  ombi la  CDU.

Kansela  ameieleza  kuwa ni  jukumu  lake  kuleta uthabiti  wa  kisiasa  nchini Ujerumani. "Dunia  haitatusubiri," ameonya.

Merkel  pia  alifananisha  kati  ya  hali  ya  baadaye  ya  Ujerumani  na  ile  ya Umoja  wa  Ulaya, akiyataka  mataifa 27 wanachama  kushikamana  kama jamii  moja.

Angela Merkel und Emmanuel Macron
Kansela Merkel (kulia) akiwa na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron(kushoto)Picha: imago/Reporters

"Hii  itakuwa  suala  muhimu  kwa  miaka  michache  ijayo," amesema.  Licha ya  hali  yake ya shaka  shaka  kisiasa  nyumbani, Merkel alionesha  mtazamo wa  mbali  katika  hotuba  yake  ya  mwaka  mpya, akiweka  malengo  kwa  ajili ya  miaka  10  hadi 15  ijayo, ikiwa  ni  pamoja  na  kuhakikisha  nafasi zilizopo  za  kazi zinaendelea  kuwapo, kutengeneza  nafasi  mpya  za  kazi, kuhimiza matumizi ya  kidigitali na  kuhimiza  usawa.

"Mambo yatakwenda  vizuri  tu kwa  Ujerumani  wakati  mafanikio  yetu yatakapomsaidia  kila  mtu, na  pale  yatakapoboresha  na  kunufaisha maisha  yetu," amesema, kabla  ya  kuwatakia  afya  njema  wananchi  na matumaini  kwa  mwaka  2018.

Mwandishi: Sekione  Kitojo / dpae

Mhariri: Isaac Gamba