1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SANTIAGO: Augusto Pinochet amepewa kaida ya mwisho hospitalini

3 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCmu

Dikteta wa zamani wa Chile,Augusto Pinochet yu mgonjwa mahututi baada ya kupata shtuko la moyo jana usiku.Kwa mujibu wa duru ya hospitali,Pinochet mwenye miaka 91 yupo katika hospitali ya kijeshi katika mji mkuu Santiago na hali yake ni mbaya sana lakini imedhibitiwa.Pinochet alieshtakiwa mauaji na utekaji nyara wa wapinzani wake wa kisiasa wakati wa utawala wake wa miaka 17,alikamatwa mara kadhaa kwa uhalifu unaosemekana kutokea wakati wa utawala wake,lakini hakuna kesi iliyosikilizwa. Kiasi ya watu 3,000 ama waliuawa au walipotea, wakati wa utawala wa jemadari wa zamani Pinochet. Vile vile zaidi ya watu 28,000 waliteswa,baada ya kiongozi huyo kushika madaraka.