1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sarri: Siubadilishi mchezo wangu licha ya kichapo cha City

Bruce Amani
11 Februari 2019

Kocha Maurizio Sarri kwa mara nyingine ameapa kutoubadilisha mfumo wake wa uchezaji kandanda licha ya vijana wake kupewa kipigo kikubwa zaidi kuwahi kuwakumba tangu 1991

https://p.dw.com/p/3DABU
Maurizio Sarri Fußballtrainer
Picha: picture-alliance/empics/S. Heavey

Mashabiki halisi wa Chelsea nadhani hawangependa kusikia tena habari hizi lakini baada ya maangamizi ya jana uwanjani Etihad..Kocha Maurizio Sarri kwa mara nyingine tena ameapa kutoubadilisha mfumo wake wa uchezaji kandanda licha ya vijana wake kupewa kipigo kikubwa zaidi kuwahi kuwakumba tangu mwaka wa 1991.

Kipigo cha Chelsea cha 6 – 0 katika Premier League mikononi mwa Manchester City kinatia wasiwasi lakini takwimuza matokeo ya timu hiyo katika mechi za ugenini zinatia wasiwasi hata Zaidi. Wameshindwa katika mechi nne mfululizo za ugenini bila kufunga bao. Hata hivyo hayo hayamtishi kocha wao Muitaliano Sarri. "Kwa sasa sijui nini sababu ya matokeo haya mabaya lakini nastahili kulifanyia kazi kwa sababu lengo langu ni kucheza kandanda langu. Sio kubadilisha mtindo mwingine wa mchezo kwa sababu kwa sasa tunacheza mpira mwingine". Amesema Sarri

Wakati Pole Gunnar Solskjaer alichukua usukani kutoka kwa Jose Mourinho katika Manchester United mwezi Desemba, ilionekana kuwa Chelsea walikuwa wakipambana na Arsenal tu, kuwania nafasi ya nne bora, huku vijana wa Sarri wakiwa pointi tatu mbele ya Arsenal na 11 mbele ya United. Lakini baada ya majanga ya jana uwanjani Etihad, United wako nafasi ya nne, pointi moja mble ya Arsenal na Chelsea.

Lakini licha ya kuwa chini ya shinikizo kubwa, Sarri anaonekana kuwa na mshirika wa karibu. Pep Guardiola. "nimesema ara nyingi, na watu hawaamini jinsi ilivyo vigumu kukifanya kitu. Mwaka wangu wa kwanza ulikuwa mgumu pia. Mwaka wangu wa kwanza, hatungecheza namna tulivyocheza. Mara nyingine tulicheza vizuri lakini bila muendelezo.  Watu hutarajia tu kocha awali na kuwanunua wachezaji na kuleta mafanikio. Inahitaji muda.

Suala la muda hata hivyo ni kitu ambacho mabosi wa Chelsea huwa hawampi mtu aliyekalia kiti moto. Wamekuwa na makocha wanane tofauti katika chini ya miaka nane.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Josephat Charo