1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Saudi Arabia inafikiria kuongeza kiwango cha uzalishaji wa mafuta

16 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CqD8

RIYADH:

Saudi Arabia imetoa ishara kuwa iko tayari kuongeza uzalishaji wa mafuta mwaka huu.

Waziri wa mafuta Ali al-Naimi amesema kuwa kwanza atazusha mjadala kuhusu jambo hilo katika mkutano ujao wa mataifa yanayozalisha mafuta kwa wingi duniani wa OPEC mjini Vienna wa mwezi Febuari. Rais wa Marekani -George W. Bush, aligusia wasiwasi wa kupanda kwa bei ya mafuta wakati wa ziara yake katika mashariki ya kati.Miongoni mwa masuala mengine yaliyotiliwa umuhimu katika ziara ya Bw Bush ni mchakato wa amani kati ya Wapalestina na waIsrael pamoja na mpango wa Iran wa Nuklia.Ziara yake hii ya Mashariki ya kati inakamilishwa leo jumatano kwa kutembelea Misri.