1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Schumacher aonyesha dalili za kurejesha fahamu

4 Aprili 2014

Michael Schumacher sasa anaonyesha “dalili za kurejesha fahamu“ ikiwa ni zaidi ya miezi mitatu baada ya kupata majeraha ya kichwa kufuatia ajali iliyomkumba katika mchezo wa kuteleza juu ya barafu.

https://p.dw.com/p/1BcGx
Michael Schumacher Porträt
Picha: Mark Thompson/Getty Images

Hayo ni kwa mujibu wa meneja wa dereva huyo wa zamani wa Formula One, Sabine Kehm. Mjerumani huyo mwenye umri wa miaka 45, alianguka wakati akiteleza juu ya barafu nchini Ufaransa mnamo Desemba 29 na akagonga upande wa kulia wa kichwa chake kwenye jabali, na akavunja helmeti yake. Madaktari walimfanyia upasuaji na kutoa mgando wa damu kutoka kwenye ubongo wake, lakini baadhi ya damu ikawachwa kwa sababu ilikuwa ndani sana ya ubongo.

Hali ya Schumacher ilibakia imara baada ya kupewa dawa za kupoteza fahamu. Mwishoni mwa mwezi wa Januari, madaktari katika hospitali moja ya mjini Grenoble nchini Ufaransa wakaanza mchakato wa kuondoa dawa hizo ili kumrejeshea fahamu. Meneja wake Sabine Kehm amesema Schumacher anaendelea vyema kwa sababu anaonyesha dalili za kupata fahamu.

Timu ya Mercedes imeanza msimu mpya wa 2014 wa Formula One kwa kishindo
Timu ya Mercedes imeanza msimu mpya wa 2014 wa Formula One kwa kishindoPicha: Reuters

Amesema yeye pamoja na familia ya Schumacher hawanuii kufichua maelezo zaidi kuhusiana na hali yake, ili kuheshimu usiri wake pamoja na familia yake na kuwawezesha madaktari kufanya kazi yao kwa utulivu.

Katika habari nyingine za Formula One, madereva wa timu ya Mercedes Lewis Hamilton na Nico Rosberg wameuanza msimu vyema baada ya kutumia muda wa kasi sana katika mazoezi ya jana kabla mashindano ya mkondo wa Bahrains Grand Prix hapo kesho Jumapili.

Hamilton alishinda mkondo wa Malaysia wikendi iliyopita, wakati Rosberg akishinda ile wa Australia. Fernando Alonso wa Ferrari alimaliza wa tatu katika mazoezi ya hapo jana. Mjerumani Sebastian Vettel ambaye ni bingwa mara nne wa ulimwengu, aliendelea kufanya vibaya msimu huu,

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman