1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sebastian Coe kugombea urais wa IAAF

28 Novemba 2014

Mtu aliyeandaa kwa mafanikio Michezo ya Olimpiki ya London mwaka wa 2012, amezindua kampeni yake ya kuwania urais wa shirikisho la riadha ulimwenguni, mojawapo ya nyadhifa kuu kabisa katika ulimwengu wa michezo

https://p.dw.com/p/1Dweg
Sebastian Coe und Jacques Rogge
Sebastian Coe na Jacque RoggePicha: Getty Images

Mshindi mara mbili wa dhahabu katika michezo ya Olimpiki Sebastian Coe amethibitisha kuwa atagombea wadhifa wa rais wa IAAF, wakati Lamine Diack wa Senegal atakapojiuzulu mwaka wa 2015.

Coe amehudumu kama makamu wa rais wa IAAF tangu mwaka wa 2007, na atazindua manifesto yake ya uchaguzi na malengo yake katika mchezo wa riadha na shirikisho linalousimamia katika wiki kadhaa zijazo.

Muingereza huyo mwenye umri wa miaka 58 amesema anataka kuwalenga vijana na uelewa wa kweli wa mazingira ya ulimwengu ambayo yanakikabili kizazi kijacho cha wanariadha na mashabiki. Coe anatarajiwa kukabiliwa na upinzani wa wadhifa wa urais kutoka kwa aliyekuwa bingwa wa Ukraine wa kuruka kwa upondo yaani pole vault Sergey Bubka.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/Reuters
Mhariri: Josephat Charo