1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sebastian Hoeness ateuliwa kuwa kocha wa Hoffenheim

Bruce Amani
27 Julai 2020

Sebastian Hoeness, mtoto wa mshambuliaji wa zamani wa Ujerumani Dieter Hoeness na mpwa wa rais wa zamani wa Bayern Munich Uli Hoeness, ameteuliwa kuwa kocha wa Hoffenheim

https://p.dw.com/p/3fzpe
Trainer Sebastian Hoeneß
Picha: Imago Images/foto2press/S. Leifer

Sebastian Hoeness, mtoto wa mshambuliaji wa zamani wa Ujerumani Dieter Hoeness na mpwa wa rais wa zamani wa Bayern Munich Uli Hoeness, ameteuliwa kuwa kocha wa Hoffenheim.

Klabu hiyo ya Bundesliga imesema Hoeness atapewa mkataba wa miaka 3 hadi 2023. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 38 anajiunga na Hoffenheim akitokea timu ya akiba ya Bayern ambayo aliiongoza kubeba taji la daraja la tatu msimu uliopita. Anachukua nafasi ya Alfred Schreuder aliyeondoka mwezi uliopita. Hoffenheim ilimaliza msimu katika nafasi ya sita.

dpa