1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SEOUL:Rais wa Korea Kusini akataa ombi la kurefusha ziara yake

3 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/CBKZ

Rais wa Korea Kusini Roh Moo-Hyun anakataa ombi la kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Il la kurefusha ziara yake kwa siku moja mjini Pyongyang.Hii ni mara ya pili kwa viongozi wa mataifa hayo kukutana katika kipindi cha miongo sita.Mkutano huo unaopangwa kumalizika hapo kesho huku Rais Roh Moo-Hyun na mwenzake wa kaskazini wanatarajiwa kutangaza matokeo .

Ombi hilo la kuongeza ziara hiyo kwa siku moja linatopa ishara nzuri na hatua ya Bwana Roh ya kukataa haieleweki.Kulingana na picha za televisheni Rais Roh Moo-Hyun alishangazwa wakati ombi hilo lilipotolewa.Kiongozi huyo alisema kuwa sharti ashauriane na idara ya usalama na itifaki.

Bwana Roh alieleza kikao chao cha asubuhi kuwa cha wazi na kuaminika ila wanapaswa kujifunza kuaminiana.Aliongeza kuwa hawakubaliani katika masuala mengi ila kuna nia ya kutaka kudumisha amani na kupanga mikakati ya baadaye.

Viongozi hao wawili waliafikiana kuwa na ushirikiano zaidi wa kibiashara na miradi ya miundo mbinu.