1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sera za Trump za uzalendo hazibadiliki

Sekione Kitojo
1 Februari 2018

Magazeti  ya Ujerumani yamezungumzia  hotuba ya rais Donald Trump wa Marekani kuhusu hali ya taifa, mazungumzo ya kuunda  serikali ya mseto nchini Ujerumani, pamoja na ziara ya waziri  Sigmar Gabriel nchini Israel. 

https://p.dw.com/p/2rtXo
USA Donald Trump Rede zur Lage der Nation
Picha: Reuters/W. McNamee

Mhariri  wa  gazeti  la Saarbrücker Zeitung anaandika  kwamba  kuna ujumbe  wa  aina  mbili , ambao Donald Trump  aliutuma: Marekani imo  katika  njia  sahihi,  na  Marekani  sio  tu imara, lakini  pia  iko tayari  kutumia  nguvu  zake. Mhariri  anaendelea:

Rais wa  marekani anapaswa  kutambua  kwamba  hali  hii inatokana  tu  na mabadiliko  ya  uongozi  katika  Ikulu  ya  Marekani ya  White House. Ni  mtazamo  wa  mtu  anayejipenda  binafsi, ambaye  kila  mara  hujiweka  mbele  kwa  kila  kitu.  Kama ilivyokuwa  kwa  mmoja  kati  ya  wangulizi  wake , hususan George W. Bush  ambaye  anamkaribia , anaelekea  katika  mwendo  wa kuyumba yumba. Ni matarajio  yetu, kwamba  hataifuata kwa  muda mrefu  njia  ya  nchi  aitakayo.

''Mtu  aliyejifunika  joho la  hamasa za uzalendo , ameelezea  kwa hali  ya  kufadhaisha  hali  ya  taifa'' Mhariri  wa  gazeti  la  Berliner Zeitung  anaandika. Nusu  karne  baada  ya  kuuwawa  kwa  Martin Luther King Marekani  imegawika  kuliko  wakati  mwingine  wowote. Hili  si  kosa  pekee  la  Donald Trump. Mhariri  anaendelea:

Siasa zake  za  mikakati  ya  matumizi ya  kimabavu  na  uongo zinaonekana  kila  siku.  Hotuba yake  ya  dakika 80  siku  ya Jumapili  katika  baraza la  Congress haziwezi  kabisa  kubadilika.

Gazeti  la  Neue Osnabrücker Zeitung  linazungumzia  kuhusu muungano  mkuu , katika  majadiliano  ya  kuunda  serikali  ya  mseto nchini  Ujerumani kati  ya  vyama  ndugu  vya  CDU/CSU pamoja  na kile  cha  kisoshalist  cha  SPD. Mhariri  anaandika kwamba kutokana  na ongezeko  la  wazee  nchini  Ujerumani  wafanyakazi wengi  zaidi  wa  kuwahudumia wazee ni  lazima  waongezeke. Hayo ni  kwa  mujibu  wa  majadiliano  yanayoendelea  ya  kuunda  serikali ya  mseto. Mhariri  anaendelea:

Haya  ni  maendeleo  yaliyotakiwa  kufanyiwa  kazi  tangu  muongo mmoja  uliopita. Lakini  sasa  yanapaswa  kutekelezwa. Pamoja  na hayo  mabadiliko  haya  yanahitaji  muda . watapatikana  wapi  mara moja  wafanyakazi 8,000, ambao  kupitia  mpango  huo  wa  haraka wataweza  kuajiriwa. Kwa  hiyo  itachukua  muda , hadi  pale wafanyakazi  wapya  watakapopata  mafunzo. Kwa  malipo  bora itawezekana  kazi  hiyo  ya  kuwahudumia  wazee  ikawavutia  watu tena. Kile  ambacho vyama  vinavyotaka  kuunda  muungano vimekinyamazia , ni  zitatoka  wapi  fedha  za  kugharamia  malipo ya  juu  ya  wafanyakazi  katika  sekta  hiyo ya  kuwapa huduma wazee.

Kuhusu  Ziara  ya  waziri  wa  mambo  ya  kigeni  wa  Ujerumani nchini  Israel, gazeti  la  Badische Zeitung  la  mjini  Freiburg linaandika.

Kitojo:

Mwaka  uliopita  baada  ya  kutokea  hali  ya  kutokuelewana mazungumzo  kati  ya  waziri  wa  mambo  ya  kigeni  wa  Ujerumani na  waziri  mkuu  wa  Israel Benjamin  Netanyahu  karibu  yavunjike kabisa.  Kwa  kutumia  busara , Gabriel  hakukata  tamaa , badala yake   alilizunguka suala  la  kuwapo  mataifa  mawili   na kuzungumzia  suala  la  ushawishi  wa  Iran  katika  eneo  hilo. Anapozungumza  Netanyahu , Israel  haisaidiki.

 

Mwandishi: Sekione  Kitojo / Inlandspresse

Mhariri: Gakuba, Daniel