1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serbia yaonya kutojiunga na Muungano wa Ulaya kuhusu Kosovo

28 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/ChRb

BELGRADE:

Serbia imetishia kufiria upya ombi lake la kujiunga na umoja wa Ulaya ikiwa umoja huo utalitambua jimbo lake la Kosovo kama taifa huru.

Bunge la Serbia limepiga kura kuunga mkono pendekezo linalosema kuwa Belgrade haitasaini mkataba wowote ule ambao hauta heshimu mipaka yake na uhuru wake kuhusiana Kosovo.Viongozi wa ki albania wa Kosovo wamesema watajitangazia uhuru mapema mwaka ujao.Baadhi ya nchi za Umoja wa Ulaya pamoja na Marekani zimesema zitawaunga mkono katika hatua yao hiyo.