1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali na AL Sadr wakubaliana juu ya kumaliza mapigano Baghdad

11 Mei 2008

-

https://p.dw.com/p/DxyM

BAGHDAD

Serikali ya Iraq na kiongozi wa kidini wa madhehebu ya washia Muqtada al Sadr wamekubaliana kumaliza mapigano ya wiki kadhaa ambayo yamesababisha kuuwawa kwa mamia ya watu katika eneo la Sadr City mjini Baghdad.Kwa mujibu wa makubaliano hayo ambayo yanaanza kutekelezwa leo hii jeshi la Mehdi ambalo ni la Sadr litaweka chini silaha,na kuwaondoa askari doria wake pamoja na mabomu yaliyotegwa katika barabara ya kuingia mji wa Sadr.Wakati huohuo wanajeshi wa Iraq na Marekani wameanzisha opresheni kubwa ambayo inalenga kuwatimua wapiganaji wa Alqaeda katika mji wa Mosul.