1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali ya Italy ya Prodi yakabiliwa na changamoto baada ya waziri mmoja kujiuzulu

22 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CvvR

ROMA:

Serikali ya Italy inayoongozwa na waziri mkuu Romano Prodi inayumbayumba kutokana na kujiondoa kwa mshirika muhimu wa serikali yake.-Waziri wa zamani wa sheria-Clemente Mastella amejiuzulu na kukiondoa chama chake kutoka kwa serikali wiki iliopita,baada ya kuchunguzwa kutokana na rushwa.Hatua hiyo imeiacha serikali ya ushirika ya Prodi bila ya wingi wa viti bungeni.Amefanya mkutano wa dharura na baraza lake la mawaziri na pia anatarajiwa leo kulihutubia bunge.