1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali ya Kenya yatakiwa kubadili sheria kuwalinda walemavu wa ngozi

Josephat Nyiro Charo23 Agosti 2010

Wito huo umetolewa kufuatia kisa cha mtu wa ulemavu wa ngozi kuuzwa na rafikiye huko Tanzania

https://p.dw.com/p/OuJO

Nchini Kenya,shirika linalowaleta pamoja watu walio na ulemavu wa ngozi limeitaka serikali kuibadili sheria inayoyatetea maslahi ya watu walio na ulemavu na kuwajumuisha. Kauli hizo zimetolewa baada ya mtu mmoja,mkaazi wa mji wa Kitale, aliye na ulemavu wa aina hiyo aliponusurika na kuponyoka kwenye mikono ya wachawi.Inaripotiwa kuwa rafikiye ndiye aliyeipanga njama hiyo ya kumuuza kwa wachawi wanaoaminika kuvitumia viungo vya mazeruzeru kutengenezea dawa au kujiongezea neema. Mtu huyo tayari ameshakamatwa na amehukumiwa kifungo cha zaidi ya miaka kumi jela nchini Tanzania alikopanga kuviuza viungo hivyo. Kufuatia tukio hilo shirika la watu walio na ulemavu wa ngozi nchini Kenya limetoa ilani kuwa usalama wako uko hatarini.

Ili kupata ufafanuzi kamili Thelma Mwadzaya amezungumza na Alex Kayolu, mwanachama wa shirika la watu walio na ulemavu wa ngozi nchini Kenya.