1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

serikali ya mseto Ujerumani

7 Oktoba 2009

Mazungumzo yaelekea wapi ?

https://p.dw.com/p/K0zQ
Bendera za CDU na FDP(Nyeusi na manjano)Picha: dpa

Maoni ya wahariri wa magazeti ya Ujerumani leo yamechambua mada mbali mbali nyingi zikiwa za ndani ya nchi: zimeanzia sera za Umoja wa Ulaya kuhusu wakimbizi,bima ya afya nchini, uhuru wa kusema Ujerumani hadi mazungumzo yanayoendelea ya kuunda serikali mpya ya muungano kati ya vyama vya CDU/CSU na FDP. Gazeti la WESTFALEN-BLAT laandika:

"Serikali ya muungano wa vyama vya bendera nyeusi na manjano ,si suluhisho la kujitoa kimaso-maso mfano wa ile ya muungano wa vyama vikuu iliokuwapo.Serikali hii mpya inapaswa kufanya mengi zaidi kuliko maswali machache tu washirika wanayoafikiana.Hakuna nafasi ya kushindwa. Kwani, vyama vya CDU/CSU na cha kiliberali cha FDP, vinapaswa kuthibitisha kuwa soko huru na serikali ni mambo yanayoweza kuunganishwa pamoja kama uhuru na usalama.Vyama hivyo vinavyopepea bendera nyeusi na manjano, vinapaswa kupambana na athari za msukosuko wa uchumi uliotokea na pia kufikiri mbali zaidi."

Likiendeleza mada hii, gazeti la FINANCIAL TIMES DEUTSCHLAND,laandika kwamba, yule alietarajia vyama vya CDU/CSU vingeachana na tabia ya kutoonesha ujasiri mara tu majadiliano ya kuunda serikali kuanza,huyo alihadaika.

Gazeti laongeza:

"Kwani ,ni kinyume chake kuona hali ya kipumbavu imezuka:Chama cha FDP ndicho kinachotoa madai na kile cha CDU, kimebaki kupinga tu.Iwapo ni kuhusu sawali la malipo kwa raia, la kuufuta kabisa mfuko wa kugharimia bima ya afya ,la kuimarisha kinga ya data za wananchi au hata kurahisisha kodi za mapato, vyama vya CDU na CSU vimebakia kusema la tu...."

WAKIMBIZI:

Likitugeuzia mada, gazeti la Braunschweiger Zeitung, linazungumzia sera ya Umoja wa Ulaya juu ya wakimbizi: Laandika:

"Katika pwani ya Watten, mkoani Lower Saxony, haikupotelea huko marekebu ya waafrika waliokonda kwa njaa na wenye kiu.Bahati gani hiyo njema kuwa nayo serikali ya Ujerumani ? Laiti ingelikuwa si hivyo, basi ingelazimika kutilia mkazo kuwapo kwa sera moja kwa nchi zote za Umoja wa Ulaya tangu ya hifadhi ya ukimbizi hata ya kuwahudumia wakimbizi.

Ni wazi kwamba, maalfu ya wakimbizi hao wanafunga safari kupitia bahari ya Mediterranian.Lakini maalfu hufaulu kupitia njia nyenginezo na kuingia nchi za Umoja wa Ulaya.Msukosuko katika pwani za bahari ya Mediterranian utakoma, pale serikali za Umoja wa Ulaya zitakapochukua msimamo wazi na unaofahamika."

MANENO YA KUTATANISHA:

Gazeti la ABENDZEITUNG kutoka Munich, linazungumzia matamshi ya diwani wa zamani wa serikali ya mkoa wa jiji la Berlin, Thilo Sarrazin juu ya waturuki humu nchini.Laandika:

"Swali nini mtu anaruhusiwa hapa kwetu kusema na nini haruhusiwi , ni mkasa wa kipekee: Wanasiasa wengi wameandamwa na kulinganishwa na Manazi.Sasa, diwani huyu wa zamani wa jiji la Berlin na kigogo cha Banki Kuu ya Ujerumani,anatiwa msukosuko kwa matamshi aliotoa juu ya waturuki.

Anaesoma mahojiano ya Bw.Sarrazin,anakuta matamshi ambayo katika majadiliano ya kistaarabu hayastahiki kuibuka kabisa: mfano, wasichana waliovaa hijabu.....Ni maneno ambayo kimsingi ,ni ya dharau .."

Muandishi:Ramadhan Ali /DPA

Mhariri: Abdul-Rahman