1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali ya umoja wa taifa inatazamiwa kutangazwa leo mjini Nairobi

Hamidou, Oumilkher6 Aprili 2008
https://p.dw.com/p/Dcxl

Nairobi:

Rais Mwai Kibaki wa Kenya na Raila Odinga anaetazamiwa kukabidhiwa wadhifa wa waziri mkuu,wamekutana kwa zaidi ya saa nne hii leo kwa lengo la kumaliza hitilafu za maoni kuhusu kuundwa serikali ya muungano nchini humo.Televisheni za Kenya zimesitisha vipindi vyote vya jumapili na kuelekeza kamera zao katika ofisi ya rais mjini Naierobi,mazungumzo hayo muhimu yanakofanyika."Viongozi wawili wanakutana na tunasubiri kuona kama serikali itatangazwa hii leo" amesema hayo msemaji wa serikali Alfred Mutua mbele ya maripota wa shirika la habari la Ufaransa AFP.Mabwana Mwai Kibaki na Raila Odinga walifikia makubaliano February 28 iliyopita,chini ya upatanishi wa mjumbe maalum wa umoja wa Afrika,Kofi Annan,ya kuunda serikali ya muungano-makubaliano yaliyodihinishwa na bunge la Kenya march 18 iliyopita.Makubaliano hayo yanazungumzia juu ya kuundwa kwa mara ya kwanza nchini Kenya wadhifa wa waziri mkuu.Serikali hiyo itakua na jukumu la kuyapatia ufumbuzi matatizo ya kijamii yanayoikumba nchi hiyo.