1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shaka kwa usalama wa vyakula Arusha

Admin.WagnerD9 Novemba 2012

Kuna habari za kutia wasi wasi kwamba baadhi ya wakulima nchini Tanzania wanatumia vumbi la madini ya uraniumu ili kuhifadhia mazao yao kama vile nafaka na matunda. Kwa mujibu wa mbunge wa Ujerumani Ute Koczy .

https://p.dw.com/p/16gHH
Demonstration unter dem Eggeturm auf dem Preussischen Velmerstot fuer und gegen den geplanten Nationalpark Teutoburger Wald-Eggegebirge-Senne: Die Bundestagsabgeordnete Ute Koczy (Kreis Lippe, Buendnis90/Die Gruenen) / people demontrating for and against the planned National Park in Teutoburger Wald - Eggegebirge - Senne / Foto: Robert B. Fishman, ecomedia, 15.4.2012
Mbunge wa Ujerumani Ute KoczyPicha: picture alliance /Robert B. Fishman/ecomedia

Mbunge huyo wa chama cha kijani nchini Ujerumani Ute Koczy ametahadharisha kwamba matumizi ya vumbi la madini ya Uranium kwa ajili ya kuhifadhia mazao ya kilimo yanaweza kusababisha hatari kubwa kwa wakulima.

Kutokana na hatari kubwa iliyopo mbunge huyo amesema pana haja kwa serikali ya Tanzania kuchukua hatua, angalau kwa ,kutoa habari kwa ukamilifu, "Sisi tunaona pana umuhimu mkubwa kwa serikali ya Tanzania na taasisi mbalimbali kulishughulikia suala hilo.Serikali na taasisi zinapaswa kutoa habari kwa ukamilifu ili watu wajue ni nini kinaweza kutumika na nini kinapaswa kuachwa."

Kwa muda wa miaka mingi mbunge huyo wa Ujerumani Ute Koczy ambae ni msemaji wa wabunge wa chama cha kijani juu ya masuala ya maendeleo amekuwa anafuatilia kwa undani shughuli zinazohusu uzalishaji wa madini ya uranium nchini Tanzania. Na hivi karibuni alikuwaa nchini Tanzania ambako aliweza kuijionea mwenyewe shughuli zinazohusu uzalishaji wa madini ya uranium . Kutokana na hatari ya vumbi la madini hayo linalotumiwa na baadhi ya wakulima nchini Tanzania, mbunge huyo ameandika barua kwa Shirika la kudhibiti matumizi ya nishati ya nyuklia, na pia kwa Rais na Waziri Mkuu wa Tanzania. Jee ni nini hasa anata katika barua alizoandika? "Nionavyo mimi pana mambo ya kichini chini yanayotokea. Tunaingiwa wasiwasi tunaposikia kwamba wakulima nchini Tanzania wanaanza kutumia vumbi la madini ya uranium ili kuhifadhia mazao yao.Sasa tunaanza kujiuliza jee kinatokea nini nchini Tanzania? alisema mbunge huyo.

A farmer prepares water channels in his maize field in Ngiresi near the Tanzanian town of Arusha on Tuesday, July 17, 2007. Millions of farmers around the world will be affected by a growing movement to change one of the biggest forces shaping the complex global food market: subsidies. Many experts agree farmers need help to grow food year in and year out, but Western farmers may get too much and African farmers too little. (AP Photo/Karel Prinsloo)
Mkulima mkoani ArushaPicha: AP

Mbunge huyo wa Ujerumani bibi Ute Koczy aliongeza kusema ni hatari kubwa kwa wakulima na kwa watu wengine nchini Tanzania kukaribiana na vumbi la madini ya uranium.

Aidha alisema mpaka sasa hakuna data na takwimu zinazofahamika juu ya viwango vya miali inayoweza kuwa hatari.Kuna habari zinazopingana juu ya hayo. Kutokana hali iliyopo mbunge huyo anataka kupigwa marufuku kabisa kwa matumizi ya vumbi la uranium nchini Tanzania.

Hata hivyo ni vigumu kwa mbunge huyo kusema ni kiasi gani cha vumbi la uranium kinachohusika kwa jumla. Lakini amesema mashirika yasiyo ya kiserikali yameteoa tahadhari na shirika la nishati ya kiatomiki la Tanzania pia limethibitisha habari hizo.

Mwandishi:Mtullya abdu/Mahojiano Schmidt Andrea.
Tafsiri:Mtullya abdu.
Mhariri:Abdul-Rahman