1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shambulio la mjini London ni shambulio dhidi ya Ulaya

Sekione Kitojo
20 Juni 2017

Mtu mmoja aliendesha gari na kugonga kundi la waumini wa Kiislamu mjini London, na kusababisha mtu mmoja kufariki na wengine kadhaa kujeruhiwa Uhalifu wake aliofanya ni usaliti kwa maadili ya Ulaya; DW: Kersten Knipp.

https://p.dw.com/p/2f0U3
England London Finsbury Park Moschee mutmaßlicher Anschlag auf Muslime
Picha: Reuters/H. Mckay

Dereva wa  gari nyeupe  ya  kusambaza  mizigo  ambayo  iligonga kundi  la  Waislamu  ambao  walikuwa  wanatoka  tu  katika  msikiti wao  usiku  wa  Jumapili anafurahishwa  kabisa  na  hatua  yake aliyochukua. "Nimefanya wajibu wangu," anaripotiwa  kusema  hivyo kwa  mtu mmoja  aliyeshuhudia  baada  ya  kutoka  katika  gari  yake. Jukumu  lake : shambulio la  kiwoga dhidi  ya  watu ambao hawakuweza  kujitetea waliokuwa  wanatoka  kutoka  katika  ibada.

Huenda  hatujui mengi kuhusiana  na  mshambuliaji  mwenyewe. Lakini  kile  tunachojua  kwa  hakika ni  kwamba  aliwahi  kufanya uhalifu  mkubwa  kabisa , shambulio dhidi  ya  watu  kwa  jumla , ambao  wanajitambulisha  moja  kwa  moja  na  kundi  lao. hapa ni  , Waislamu. Bila  shaka  hii  ni Chuki  na  uhalifu , kwa  hali isiyoeleweka , na  pia  ni  shambulio  la  kisiasa  ambalo ni  chini kabisa  ya  kiwango  chochote cha  ustaarabu wa  aina  yoyote.

Kwa  maneno  mengine , hili  lilikuwa tukio  ambalo  halina  tofauti  na shambulio lililofanywa mara  kadhaa  katika  miezi  iliyopita  na miaka  na  watu wa kundi  la kigaidi  linalojiita Dola  la  Kiislamu , IS.

Uhalifu  wao  pia  ni  wenye sura ya  uwoga na uovu  tu. Kundi  la  IS ni  kundi  linafanya  unyama  bila  kujali maadili  ama  viwango vya kisiasa.

Knipp Kersten Kommentarbild App
Mhariri Knipp Kersten

Hii  ndio  sababu  magaidi  wanafanya  mambo  yao  kama  yule aliyefanya kitendo  cha  mauaji  mjini  London  ambapo  ni  kinyume kabisa  na  msimamo  wa  kimaadili, na  pia  ni  maafa  kwa ustaarabu. Watu  wanaofanya  mambo  kama  aliyofanya mshambuliaji  huyo  na  gari  yake  wako tayari  kutumbukia  katika kiwango  kama  cha  IS, kiwango  cha  wakorofi dhalili na walioshindwa  maisha, vijana, ambao  wanaendeshwa  na  hamasa , bila  kuwa  na  uwezo  wa  kudhibiti  nafsi  zao  ama  uwezo  wa uzalishaji  katika  jamii.

Nguvu  za  kibinadamu  zinazolisha  kundi  la  IS  zimejaa watu wenye  hasira  duniani  kote, watu  wenye  mtazamo  wa  uharibifu, hisia  za  kuuwa  na  ambao  huhisi  kuhalalishiwa  na  propaganda inayotolewa  na  magaidi  wa  kundi  la  IS.  Ulaya  iliyostaarabika haipaswi  kufanya  hivyo.

Ndio , Ulaya  ni  bara  ambalo  linahistoria  ya  kumwaga  damu. Lakini  pia  ni  bara  la  ustaarabu. Kanda  ambayo , licha ya makosa  yote  mabaya  ambayo  inapaswa  kuwajibika, uvamizi  wa Iraq  mwaka  2003 miongoni  mwa  mengine,  kila  mara  inawajibika na  inataka  kujifunza  kutokana  na  kujitazama  na  kujikosoa. Ulaya imeweka  kiwango  cha  juu cha  maadili kwake  binafsi. Maadili  yetu yanataka  kwamba  tuzungumze  baina  yetu , na  sio  kupigana miongoni  mwetu na  sio  kuwafanyia  ugaidi  wengine kwa  misingi ya  chuki.

Mwandishi: Kersten Knipp  / ZR / Sekione  Kitojo

Mhariri: Yusuf Saumu