1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shambulizi la kemikali Syria"uongo" mtupu-Assad

Jane Nyingi
13 Aprili 2017

Jeshi la Syria  limesema vikosi vya Marekani vimewaua mamia ya watu  baada ya kushambulia ghala moja la kuhifadhi kemikali linalosimamiwa na wapiganaji  wa IS.Shambulizi hilo la angani lilifanywa mkoa wa Deir al Zor.

https://p.dw.com/p/2bDLy
Syrien Idlib Giftgasangriff
Picha: picture-alliance/abaca/S. Zaidan

Hayo yanajiri huku  rais Bashar al Assad akidai serikali yake ilisingiziwa kwa asilimia 100 kuwa ilihusika katika  shambulizi la sumu ya gesi mkoa wa Idlib lilosababisha maafa  ya zaidi ya watu 80. Katika mahojiano ya kipekee na  shirika la habari la AFP  katika ikulu ya rais mjini Damascus nchini Syria ,al-Assad amesema  kimaadili serikali yake haiwezi kufanya  kamwe shambulizi hatari kama hilo kwasababu halikubaliki. Kiongozi  huyo ambae anapambana katika vita vinavyonuia kumwondoa madarakani tangu taifa lake kutumbukia katika mapigano miaka sita iliyopita,amesema hatishiki na  shambulizi liloamriwa na rais wa Marekani  Donald Trump,na kukiri kuwa anatazamia kufanyika mashambulizi zaidi. Rais Assad amesisitiza kuwa vikosi vyake viliacha kutumia  silaha zote za sumu   miaka mingi iliyopita na haviwezi kutumia silaha hizo zilizopigwa marufuku. Mahojiano hayo na shirika la habari la AFP yalikuwa ya kwanza tangu kutokea  shambulizi la silaha za sumu  tarehe 4 mwezi huu lilosababisha mauji ya watu chungunzima wakiwemo watoto 31 katika mji unaoshikiliwa na waasi wa Khan Sheikhun. Rais huyo wa Syria  amesema ushahidi kuhusu shambulizi hilo ulitolewa tu na kundi la wapiganaji wa Al-Qaeda  akimaanisha lilokuwa kundi la wapiganaji ,ambalo ni miongoni mwa makundi mengine yanayosimamia mkoa  huo wa Idlib. Picha za baada ya shambulizi zilizowaonyesha waathiriwa baadhi yao watoto  waliokuwa wakitokwa na povu mdomoni ziliushtua ulimwengu mzima. Hata hivyo Assad anashikilia kusema kwamba ni vigumu kubaini iwapo shambulizi hilo lilitokea kwa kuwa hakuna  anayeweza kuithibitisha video hiyo kutokana na kuzangaa video za kutengenezwa.

Der syrische Präsident Assad gibt Interview zu dänischen TV-SenderDer syrische Präsident Assad gibt Interview zu dänischen TV-SenderDer syrische Präsident Assad gibt Interview zu dänischen TV-Sender
Rais wa Syria Bashar-al-AssadPicha: Picture-Alliance/Epa/Sana

Marekani yalaumiwa kuwaua raia

Taarifa nyingine ni kuwa serikali ya Syria imesema mashambulizi yanayofanywa na Marekani nchini humo yameendelea kuwaua mamia ya raia.Katika tukio la hivi karibuni vikosi hivyo vya Marekani vinadaiwa  kuushambulia mkoa wa Deir al Zor na kuwaua mamia ya watu wakiwemo raia. Hata hivyo  msemaji wa kikosi cha Marekani John Dorrian ameyakanusha madai hayo na kusema  si ya kweli. Hata hivyo Marekani imekiri kuwa iliwaua kimakosa wapiganaji 18 wa kikosi cha democrasi nchini Syria-SDF kufuatia shambulizi la angani. Kikosi hicho kinachowajumuisha Wakurdi  na Waarabu kinaungwa mkono na Marekani.  Hata hivyo SDF kimesema kitaendelea na harakati zake za kukabiliana na wapiganaji wa IS licha tukio hilo. Vikosi vya marekani  hata hivyo vimesema vinatathmini kilichosababisha makosa hayo ili kuzuia matukio kama hayo  kujirudia.

Syrien Weißhelme in Aleppo
Watoto walionusurika shambuliziPicha: Reuters/S. Kitaz

Mwandishi:Jane Nyingi AFP/AP
Mhariri:Yusuf Saumu