1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SHANGHAI: Matatizo ya kimataifa ni kitisho kwa dunia nzima

26 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBy2

Rais wa Ujerumani,Horst Köhler akimaliza ziara yake barani Asia,ametoa mwito wa kuwepo ushirikiano zaidi kati ya mashirika ya kiserikali kutenzua matatizo ya kimataifa.Amesema,uchafuzi wa mazingira,ongezeko la joto duniani,uhaba wa nishati na umasikini barani Afrika ni kitisho kwa nchi zote duniani.Rais Köhler,alitoa mwito huo alipohotubia Chuo Kikuu cha Tongyi mjini Shanghai.Köhler alimaliza mazungumzo yake ya kisiasa na viongozi wa China siku ya Ijumaa,mjini Beijing na amesema ameridhika.Kibiashara, Ujerumani ni mshirika mkuu wa China barani Ulaya.