1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sheria dhidi ya kuchomwa moto bendera Ujerumani

Oumilkheir Hamidou
12 Desemba 2017

Sheria maalum maandamano yanapotokea. Watu kufunika nyuso zao ili wasijulikane. Matumizi ya nguvu au vitisho ni miongoni mwa visa vinavyo vuruga amani nchini; hapa ndipo linapozuka suala la huru wa mtu kutoa maoni yake

https://p.dw.com/p/2pBtD
Deutschland Demonstranten verbrennen Fahne mit Davidstern in Berlin
Picha: picture alliance/dpa/Jüdisches Forum für Demokratie und gegen Antisemitismus e.V.

Mjadala umezuka tena kuhusu mipaka ya uhuru wa mtu kutoa maoni yake, baada ya bendera za Israel kuchomwa moto maandamano yalipozuka mwishoni mwa wiki iliyopita mjini Berlin, watu walipokuwa wakilalamika dhidi ya uamuzi wa rais Donald Trump wa Marekani wa kuutambua mji wa Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel. Visa vilivyojiri ijumaa usiku mbele ya ubalozi wa Marekani na  maandamano ya jumapili iliyopita ambapo watu wasiopungua 25 elfu waliongozana kutoka Neuköln hadi Kreuzberg, vimekosolewa vikali na watu wengi.

Msemaji wa serikali Steffen Seibert alisema wazi kabisa jumatatu kwamba uhuru wa kuandamana na kutoa maoni "haumaanishi uhuru wa visa vilivyokithiri, chuki dhidi ya wayahudi na wageni na matumizi ya nguvu."Kansela Angela Merkel pia alisema tunanukuu: "Tunapinga aina zote za chuki dhidi ya wayahudi na chuki dhidi ya wageni. Serikali inabidi itumie nguvu zote za kisheria dhidi ya visa kama hivyo."

Picha ya mwaka 1929 ya Bunge la Ujerumani-Reichtag
Picha ya mwaka 1929 ya Bunge la Ujerumani-ReichtagPicha: Imago/United Archives International

Suala linalozukla lakini ni jee  serikali ina nguvu za aina gani za kisheria?

Kuwaandamana watu mahakamani kwasababu ya kuchoma moto bendera za Israel si jambo linalowezekana. Kifungu nambari 104 cha sheria ya makosa ya jinai ingawa kinazungumzia kuhusu faini au kifungo cha hadi miaka miwili "kwa sababu ya kwenda kinyume na muongozo wa sheria au kuiharibu hadharani bendera ya nchi ya kigeni, lakini hiyo inamaanisha tu kwamba kisa kama hicho kinaweza kuhukumiwa ikiwa bendera yenyewe hasa ya nchi ya kigeni, mfano bendera iliyotundikwa katika jengo la ubalozi ndiyo iliyoharibiwa.

Lakini mwishoni mwa wiki iliyopita zilizochomwa moto ni bendera ambazo waandamanaji wamekuja nazo na baadhi wamezitengeneza wenyewe."Hapo hakuna makosa ya uhalifu" anasema Thomas Nuenddorf, msemaji wa polisi ya mjini Berlin katika mahojiano na DW:

Mmojawapo wa washirika katika maandamano ya Berlin
Mmojawapo wa washirika katika maandamano ya BerlinPicha: Reuters/A. Schmidt

Wafunguliwa kesi kwa kutotii amri ya polisi

Hata hivyo polisi wana uwezo wa kutoa amri kuwakataza waandamanaji kwa mfano wasitie moto vitu mfano wa masanamu na bendera. Atakaekwenda kinyume na amri hiyo anaweza kutozwa faini.

Na hilo hasa ndilo lililotokea katika maandamano ya ijumapili iliyopita mjini Berlin. Watu 10 waliokamatwa wakati wa maandamano hayo hawatoshitakiwa kwasababu ya kutia moto bendera bali kwasababu ya kutofuata amri ya polisi.

Mbali na kutia moto bendera, waandamanaji walipaza sauti na kuitaja Israel kuwa "ni nchi inayouwa watoto wadogo na wanawake-matamshi ambayo pia yamezusha hasira. Meya wa Berlin Michael Müller amesema polisi watafuatilizia kila kosa la jinai lililotokea.

 

Mwandishi:Hammerstein,Leonie/Hamidou Oummilkheir

Mhariri :Mohammed Abdul-Rahman