1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sheria ya kutotoka ovyo yapunguzwa makali Myanmar

14 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Fu

Rangun:

Watawala wa kijeshi wa Myanmar wamepunguza makali ya sheria ya kutotoka ovyo katika mji mkuu Rangun.Wakaazi wa mji huo wanasema wanajeshi wakitumia mabomba ya kukuza sauti,wametangaza muda wa marufuku ya kutoka saa za usiku utakua wa saa nne badala ya saa sita.Idadi ya wanajeshi wanaopiga doria nayo pia imepunguzwa.Wakati huo huo wawakilishi wa upande wa upinzani wamesema wanaharakati wanne mashuhuri wamekamatwa na polisi mjini Rangun.Wanaharakati hao ni wafuasi wa kundi la wanafunzi walioongoza maandamano ya mwaka 1988 dhidi ya serikali.Maandamano yaliyoongozwa na watawa wa kibuddha, mwezi uliopita dhidi ya utawala wa kijeshi wa Myanmar,yamegharimu maisha ya watu 13 na wengine zaidi ya elfu mbili kutiwa mbaroni.-