1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sheria ya uwekaji wa takwimu yapingwa.

1 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CieE

Kalsruhe, Ujerumani. Zaidi ya watu 30,000 wanapinga sheria mpya nchini Ujerumani ambayo itaruhusu serikali kuweka takwimu kubwa kabisa kupitia mawasiliano ya simu. Sheria hiyo ambayo inaanza kazi leo Jumanne, inahitaji mashirika ya simu kuweka rekodi zao kwa muda wa miezi sita za wapiga simu na watumiaji wa internet ikiwa ni pamoja na tarehe na muda wa matumizi na nani amempigia nani. Takwimu hizo kutoka simu za mkononi zitajumuisha maeneo na mpigaji simu. Mwanasheria ambaye amepeleka malalamiko hayo katika mahakama kuu ya katiba mjini Karlruhe pia ametaka kusitishwa mara moja kwa sheria hiyo kwa misingi kwamba inakwenda kinyume na katiba. Sheria hiyo inatekeleza maelekezo ya umoja wa Ulaya ambayo inalenga katika kupambana na ugaidi.