1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shirika la Atomic duniani lasema limefikia muafaka na Iran kuhusu Nuklia

13 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cp3F

VIENNA:

SHIRIKA la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Atomic limesema jumapili kuwa limekubaliana na Iran kwa kile lilichokiita mda wa wiki nne kuweza kumaliza masuala yote kuhusiana na mpango wa utata wa Iran wa Nuklia. Taarifa ya shirika hilo imesema kuwa wakati wa mikutano ya mkuu wa shirika hilo- Mohammed El Baradei na kiongozi wa kidini wa Iran,Ayatollah Ali Khamenei pamoja na rais Mahmod Ahmedinejad,wamekubaliana kwa mda huo wa wiki nne ili kumaliza kilichoitwa mpango wa kumaliza masuala yaliyosalia.Habari za awali zilisema kuwa Ali Khamenei alikuwa amemuambia Elbaradei kuwa Iran haitaachana na mpango wake wa nuklia kwa matumizi ya nyumbani. Mataifa ya magharibi yanahofu kuwa Tehran huenda inataka kutengeneza silaha zaNukila.Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeiwekea Iran vikwazo mara mbili kwa kushindwa kueleza wazi mpango wake wa Nuklia.