1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shirika la misaada lazishutumu nchi za magharibi kwa kutotimiza ahadi.

25 Machi 2008
https://p.dw.com/p/DUG3

Kabul.

Shirika moja la kutoa misaada la Oxfam limesema kuwa mataifa ya magharibi yameshindwa kutoa kiasi cha dola bilioni 10 zilizoahidi kuipatia Afghanistan kama msaada. Jumuiya ya kimataifa iliahidi kiasi cha dola bilioni 25 kwa Afghanistan tangu mwaka 2001.

Hata hivyo , ni kiasi cha dola bilioni 15 tu cha misaada ndio kimetumika hadi sasa, kwa mujibu wa shirika hilo la Oxfam.

Zaidi ya hayo , shirika hilo limesema kuwa kiasi hicho cha theluthi mbili ya misaada hakikutumika kupitia serikali. Shirika hilo pia linakadiria kuwa asilimia 40 ya msaada wa fedha umerejea katika nchi hizo fadhili kama faida ya makampuni na mishahara ya wafanyakazi.