1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shirika la UNHCR laitaka Afrika Kusini kuwavumilia wazimbabwe kwa muda

23 Mei 2008

-

https://p.dw.com/p/E53e

GENEVA

Shirika la Umoja wa mataifa la kuwahudumia wakimbizi la UNHCR limezungumzia wasiwasi wake kuhusu mashambulio ya chuki dhidi ya wageni nchini Afrika Kusini na kuitolea mwito serikali ya nchi hiyo kuwapa vibali vya kuishi kwa muda nchini humo wakimbizi wa Zimbabwe.

Zaidi ya watu elfu 17 wanakadiriwa kuyatoroka mashambulio katika kipindi cha wiki mbili zilizopita wakiwemo wakimbizi kutoka Zimbabwe.Ghasia dhidi ya wageni nchini Afrika Kusini zimeenea na kuingia kwa mara ya kwanza katika mji wa Cape Town na maeneo ya Durban licha ya serikali kuagiza jeshi liingilie kati kuzuia machafuko hayo.Msemaji wa shirika la UNHCR Jennifer Pagonis amesema wito wa kuitaka Afrika kusini iwape vibali vya kuishi kwa muda Wazimbabwe umetokana na kuwa hawawezi kurudi nyumbani kufuatia hali ya kisiasa ilivyo nchini mwao.Maelfu ya raia wa Msumbiji wanaendelea kurudi nchini mwao wakisaidiwa na serikali yao.Hata hivyo leo serikali ya Zimbabwe imetangaza kwamba itawasaidia raia wake walioko Afrika Kusini kurudi nyumbani na pia kurudisha maiti za wazimbabwe waliouwawa.Zaidi ya watu 40 wameuwawa na wengine elfu 16 wameachwa bila makaazi katika mashambulio hayo dhidi ya wageni nchini Afrika Kusini.