1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shirikisho la Soka Afrika lapata kiongozi mpya

Admin.WagnerD16 Machi 2017

Ahmad Ahmad wa Madagascar amechaguliwa kuwa rais wa Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) kwa kumng'oa kiongozi mkongwe Issa Hayatou baada ya kuwa madarakani kwa miaka 29.

https://p.dw.com/p/2ZLIU
Ahmad Ahmad
Picha: Getty Images/AFP/Rijasolo

Ahmad ambaye ni mkuu wa shirikisho la soka nchini Madagascar alishinda uchaguzi huo uliofanyika Alhamisi (16.03.2016)katika mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa kwa kura 34 dhidi ya 20 alizopata Hayatou.

Wajumbe walipiga ngumi zao hewani kufuatia tangazo la matokeo hayo yalioashiria kuondoka kwa kiongozi wa mwisho wa kizazi cha wazee katika ulimwengu wa soka.

Ahmad mwenye umri wa miaka 57 baba wa watoto wawili alikuwa akifundisha soka kabla kuchukuwa hatamu ya kuliongoza shirikisho la soka la Madagascar hapo mwaka 2003.Ushindi wake umewashangaza wengi wakati Hayatou alikuwa amewekewa matumaini ya kuchaguliwa tena.

 

Kufanya mageuzi

Africa Cup of Nations DR Kongo - Togo
Kabumbu la Afrika.Picha: Getty Images/AFP/J. Tallis

Ahmad amewaambia waandishi wa habari baada ya kuchaguliwa kwake kwamba unapojaribu kufanya kitu inamaanisha kwamba unaweza kufanya.Amesea ikiwa hawezi kufanya asingelisimama kuwania wadhifa huo.Awali amesema mpango wake ulikuwa ni kufanya mageuzi ya utawala wa shirikisho la soka la Afrika kuepusha kuhusishwa kwa siasa katika shirikisho hilo.

Hayatou ambaye ni mwananchi wa Cameroon amekuwa akiingoza CAF tokea waka 1988 na makamo wa rais mzee katika shirikisho la soka duniani FIFA.Anapewa sifa ya kuongeza idadi ya timu za Afrika katika michuano ya kuwania kombe la soka la dunia na kuipatia fedha za ziada michuano ya soka ya bara hilo.

George Afriyie makamo wa rais wa chama cha soka cha Ghana amesema mheshimiwa Issa Hayatou amefanya mengi kwa soka la Afrika lakini wakati umefika wa kun'gatuka.

Hayatou aliondolewa ukumbini na wasaidizi wake waliokuwa akipuuzilia mbali maombi ya wandishi waliokuwa wakitaka zungumze chochte kile wakati Ahmad alibebwa na kushangiliwa na wafuasi wake.

Utawala wa Hayatou

Zürich FIFA Interims-Präsident Issa Hayatou
Issa Hayatou aliyen'golewa.Picha: Getty Imgages/AFP/F. Coffrini

Utawala wa Hayatou katika shirikisho la soka la CAF mara nyingi umekuwa na utata ametuhumiwa na gazeti la Uingereza la Sunday Times kwa kupokea dola milioni moja na nusu kuipigia kura Qatar wakati ilipotunukiwa kuandaa michuano ya soka kombe la dunia kwa mwaka 2022 miaka saba iliopita.

Mwaka 2011 Hayatou alikaripiwa na Kamati ya Kimataifa ya Olympik kuhusiana na fedha alizopokea kutoka kampuni ya soko la michezo ISK yenye doa la kashfa.

Wakati huo huo Zanzibar visiwa vilioko mwambao wa Afrika mashariki imekubaliwa kuwa mwanachama kamili wa Shirikisho la soka la Afrika CAF.

Timu ya taifa ya Zanzibar sasa itaweza kushiriki michuano ya soka ya kombe la mataifa ya Afrika iwapo ikifuzu na michuano mengine ya timu za taifa ya CAF na chama cha soka kitakuwa na haki ya kupiga kura  katika masuala ya soka ya bara hilo.

Mwandishi : Mohamed Dahman/AFP/AP

Mhariri :Yusuf Saumu