1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shughuli za hatari za kampuni ya Blackwater.

Mtullya, Abdu Said26 Februari 2008

Licha ya kutuhumiwa kutenda uhalifu kampuni ya Blackwater haijachukuliwa hatua za kisheria

https://p.dw.com/p/DDkj
Askari wa kampuni ya Blackwater ya Marekani nchini Iraq.Picha: AP



Kampuni ya ulinzi  Blackwater ya Marekani ambayo imeajiriwa na utawala Bush kulinda usalama nchini Irak, mwaka jana  ilihusika na mauaji ya raia 17 mjini Baghdad.

Pia pana madai kwamba kampuni hiyo inajihusisha na biashara ya silaha.

Raia hao walidaiwa kuwa na nia ya kuwashambulia wamarekani.

Wairaki wengine 24  walijeruhiwa katika shambulio hilo.

Lakini tofauti na mikasa mingi mingine, tukio hilo lilizingatiwa kwenye bunge la Marekani lakini hakuna hatua yoyote thabiti iliyochukuliwa dhidi ya kampuni hiyo ya Blackwater.

Mwandishi na mchapishaji  wa  Marekani Jeremy Scahill amendika kitabu juu ya shughuli za kampuni hizo ambazo ameziita kuwa ni majeshi ya watu binafsi.