1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shule ya Kimarekani Gaza yahujumiwa

21 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC8T

GAZA:

Wapalestina wenye siasa kali, wameripua sehemu ya shule ya kimataifa ya kimarekani huko mwambao wa Gaza leo hii.Wamesababisha hasara katika jengo hilo lakin, hakuna aliedhurika.Wakuu wa shule hiyo wamearifu kwamba , wafuasi hao wameripua mabomu 3 katika majengo 2 ya shule hiyo huko kaskazini mwa Gaza.

Washambulizi hao, wamejitambulisha kuwa ni tawi la al Qaeda katika mwambao wa Gaza.

Msemaji wa Ubalozi wa Marekani amesema kuwa, shule hiyo haina mafungamano na serikali ya Marekani.